Leviticus 1:1-6

Sadaka Ya Kuteketezwa

1 a Bwana akamwita Musa na kusema naye kutoka kwenye Hema la Kukutania, akamwambia, 2 b“Sema na Waisraeli na uwaambie, ‘Yeyote miongoni mwenu aletapo sadaka ya mnyama kwa Bwana, alete mnyama kama sadaka yake kutoka kundi lake la ng’ombe au la kondoo na mbuzi.

3 c“ ‘Kama sadaka hiyo ni ya kuteketezwa kutoka kwenye kundi la ng’ombe, atamtoa ng’ombe dume asiye na dosari. Ni lazima amlete kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili aweze kukubalika kwa Bwana. 4 dAtaweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka ya kuteketezwa, nayo itakubaliwa kwa niaba yake ili kufanya upatanisho kwa ajili yake. 5 eAtamchinja yule fahali mchanga mbele za Bwana, kisha wana wa Haruni kuhani wataleta damu na kuinyunyiza pande zote za madhabahu yaliyo penye ingilio la Hema la Kukutania. 6 fAtaichuna hiyo sadaka ya kuteketezwa na kuikata vipande vipande.
Copyright information for SwhKC